ROHO MTAKATIFU NI MUNGU ANAEISHI


www.wokovukwawote.blogspot.com


Utangulizi
Ezekieli 36:27 “nami nitatia roho  yangu ndani yenu na kuwaendesha  katika sheria zangu  nanyi mtazishika hukumu zangu na kuzitenda” maneno haya anayasema MUNGU kupitia kinywa cha nabii ezekieli  na katika  kumbukumbu la torati anasema hivi Kumbukumbu la torati 4:6 anasema “sikiza ee izraeli ;Bwana, Mungu wetu,Bwana ndiye mmoja”MUNGU ni mmoja anaposema nitatia roho yangu ndani yenu (yetu) maana yake  Mungu kuja kukaa ndani yetu kupitia ROHO MTAKATIFU,biblia katika ule waraka kwanza wa yohana 4:8-9 anasema “kwa maana wako watatu washuhudiao[mbinguni Baba,na Neno,na Roho mtakatifu na hawa watatu ni umoja .9kisha wako watatu washuhudiao duniani]Roho,na maji,na damu;na hawa hupatana kwa habari moja.tukipokea ushuhuda wa wanadamu ,ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi;kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu ,amemshuhudia mwanawe.mungu mmoja aliye ziumba mbingu na nchi yeye mungu na roho mtakatifu na Neno(Yesu) mbinguni ni umoja na duniani wako watatu wanaopatana kwa habari mmoja.
Watatu duniani biblia inasema ni Roho Mtakatifu(mungu pamoja nasi),Maji, na Damu.Kwa habari ya maji biblia inasema hivi “ezekieli 36:25 nami nitawanyunyizia maji safi,nanyi mtakuwa safi;nitawatakaseni na uchafu wenu wote,na vinyago vyenu vyote” anaeleza habari ya utakaso. Damu  yaYESU ndio ukombozi na upatanisho wetu ili tumwone Mungu.    
Mungu ni mmoja na amejifunua kwetu kwa namna ya nafsi tatu
                i.            Mungu baba “atawalae yote”
              ii.            Mungu mwana “ambae vyote  katika yeye viliumbwa”
            iii.            Mungu roho mtakatifu “aangaliae yote”

MUNGU BABA
Mungu baba ndie aliyeumba vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana hakuna ubishi ndie mtawala wa vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekanavimeumbwa na yeye. Tazama kitabu cha nabii isaya 48:12-13 anasema “nisikilize mimi ee yakobo na izraeli  niliyekuita mimi ndiye wa kwanza na mimi ni wa mwisho pia naam,mkono wangu umeiweka msingi wa dunia na mkono wangu wa kuume umezitanda mbingu ;niziitapo husimama pamoja”  
MUNGU MWANA (YESU) AMBAYE VYOTE KATIKA YEYE VILIUMBWA
Waebrania 1:1-3 neno la mungu linasema “mungu baba ambaye zamani alisema zamani na baba zetu kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi mwisho wa siku hizi amesema nasi katika mwana ,aliyemweka kuwa mrithi wa yote tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.yeye kwa  kuwa mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake,akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake  akiisha kufanya utakaso wa dhambi aliketi mkono wa kuume wa ukuu huko juu”    
Pia katika waraka wa pili wa mtume Paulo kwa wakoritho anasema 2wakoritho5:19 anasema “yaani mungu alikuwa ndani ya kristo akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake,asiwahesabie makosanae ametia ndani yetu neno la upatanisho”.
YESU ni mungu kukosa kufahamu hilo ni kosa kwa sababu mungu  alimtuma mwana wake yesu kwa sababu alikuwa ndani yake kwa ROHO MTAKATIFU akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake.
v  ROHO MTAKATIFU ndiye aliyekuwa ndani ya Yesu akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake
Luka mtakatifu anasema luka 1:35 “malaika kajibu akamwambia Roho mtakatifu atakujilia juu yako na nguvu zake aliye juu zitakufunika kama kivuli kwa sababu hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu MWANA WA MUNGU”Maneno haya aliyasema malaika Gabrieli  alipokuwa akimweleza mariamu juu ya kuzaliwa Yesu na matokeo yake ilikuwa hivi “mathayo1:18 “kabla hawajakaribiana alionekana ana mimba kwa uwezo wa Roho mtakatifu”.  Mwana wa mungu yesu ni mungu na katika kitabu cha waebrania anasema waebrania 1:8 “lakini kwa habari ya mwana asema kiti chako cha enzi Mungu ni cha milele na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili”
Si wanadamu tu waliokili kuwa yesu ni mungu bali hata malaika waliotumwa na mungu walikiri kuwa yesu ni mungu “luka 1:32-33 huyo atakuwa mkuu ataitwa mwana wa aliye juu,Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake.ataimiliki nyumba ya yakobo milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho”  na tunajua ufalme wa mungu pekee ndio hauna mwisho na kupitia Yesu atamiliki nyumba ya yakobo milele na milele.twaweza sema kwamba ufalme wake hauna mwisho kwa sababu yeye ni mungu wa milele.   
Umewahi kujiuliza namna ambavyo YESU alijitambulisha kwa wanafunzi wake pale walipokuwa na mashaka naye yohana 14:9 “Yesu akamwambia mimi nimekuwaapo pamoja nanyi siku zote wewe usinijue Filipo?aliye niona mimi amemwona baba basi wewe wasemaje utuonyeshe baba”
            MUNGU ROHO MTAKATIFU
Ni Mungu aangaliae yote zaburi 139:7 inasema “niende wapi njiepushe na Roho yako,Niende wapi niukimbie uso wako”  
Ni maombi yangu  zaburi 51:11-12 inayosema “usinitenge na uso wako wala Roho yako mtakatifu usiniondolee unirudishie furaha ya wokovu wako ,unitegemeze kwa Roho ya wepesi wako” yatimie kwako.
Ø  Inawezekana moyoni mwako upo uchungu, magonjwa yanakusumbua,unateswa na majini wachawi mapepo na mizimu huoni kimbilio ila waganga wa kienyeji ,unateswa na ndoto mbaya.
Ø  Upo hapo na inawezekana hujawahi msimulia mtu mwingine yeyote namna unavyoingiliwa na mtu katika ndoto(anafanya mapenzi nawe kwenye ndoto) na hiyo hali huipendi ila huelewi ufanye nini.
Ø  Kila unalofanya halifanikiwi hamna mpenyo kila kitu unachokifanya hata kama waona ni chema lakini mwishowe kuishia kukataliwa  Jewewe una roho za kukataliwa?je unateswa na  ukichaaa,au ukimwi.
Ø  Huna mtoto madaktari hawaoni tatizo la wewe kukosa mtoto umeitwa tasa muda mrefu.
Ø  Unauvimbe ndani yako umeleta mateso,  vituvinatembea ndani yako magonjwa ya mara kwa mara tena yanayofanana na hayo
Ø  Inawezekana umetafuta kufanya urafiki na majini hata kwa kulala makaburini,umevishwa kila aina ya uchafu,kuna wakati umekula vitu ambavyo kwa hali ya kawaida huwezi kula, umeoga maji ya baharini usiku,umeoga njia panda usiku,umeoga maji ya maiti usiku lakini bado mateso yameendelea
Inawezekana kuna mambo mengi ambayo unayapitia na yameachia maumivu ndani yako mpaka kuna wakati umeona waganga wa kienyeji ndio kimbilio lakini mateso yameongezeka maradufu  waganga wa kienyeji hawana majibu wala wachawi hawawezi kukusaidia LEO NINALO  NENO JEMA KWA AJILI YAKO waliloshindwa wanadamu yupo MUNGU ANAEWEZA KUKUSAIDIA UKATOKA KATIKA HIYO SHIDA ULIYO NAYO NI YESU PEKE  YAKE AWEZA KUKUSAIDIA.
Yesu alipokuja duniani na alipokuwa anaanza kazi siku moja alijitambulisha hivi ili kujithibitisha naam kwa ajili ya hayo mateso unayopitia yesu alikuja kuyaondoa.luka4:16-19 “akaenda nazareti hapo alipolelewa;nasiku ya sabato akaingia katika sinagogi  kama ilivyokuwa desturi yake ,akasimama asome.akapewa chuo cha nabii isaya ,akakifungua chuo,akatafuta mahali palipoandikwa.Roho wa bwana yu juu yangu kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema ,amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao,na vipofu kupata kuona tena,kuwaacha huru waliosetwa na kutangaza mwaka wa bwana uliokubaliwa”
Roho mtakatifu alidhihirishwa kukomesha mateso unayopitia tena bure haulipii anachotaka kwako wewe ni  KUACHA DHAMBI NA KUMWAMINI YESU KRISTO.
BIBLIA INATUMIA MAJINA MENGI KUMTAJA ROHO MTAKATIFU
Majina yake mengi yameeleza namna anavyofanya kazi katikati yetu mfano wa majina hayo ni  
v  ROHO YA HEKIMA NA UFAHAMU ,ROHO YA SHAURI NA UWEZA,ROHO YA MAARIFA NA KUMCHA BWANA
Maisha ya mtu wa mungu kuwa na hekima  na ufahamu kuhusu mungu hutoka kwa mungu, iwe ni shauri(kusudi) na uweza katika kuuthibitisha lile shauri hutoka kwa mungu ndio maana tunasema Mungu wetu anaweza.wakristo bila maarifa kuna uangamizo na nimungu pekee ndiye atupae maarifa na ile hali ya kumhofu(kumcha) Mungu. Kupitia Mungu roho mtakatifu yote haya yamewezekana kuachiliwa ndani yetu(wanadamu)
Maandiko katika biblia yanathibitisha haya haya niliyosema hapo juu tazama “kutoka31:2-3angalia nimemwita kwa jina lake bezaleli mwana wa uri,mwana wa huri wa kabila la yuda. Name nimejaza roho ya Mungu ,katika hekima,na maarifa na ujuzi ,na mambo ya kazi ya kila aina”
Angalia tena kwa habari akina danieli na wenzake.danieli1:17 “basi kwa habari ya hao vijana wanne,Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima ;danieli alikuwa na fahamu katika maono yote na ndoto”
Inawezekana wewe pia ukatamani kuwa na maarifa,hekima ufahamu mwombe mungu ametoa kibali cha kumwomba nae atakupa sawasawa uhitaji wako yakobo1:5-6 anasema mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa mungu awapae wote kwa ukarimu ,wala hakemei ;naye atapewa ila na aombe kwa imani ,pasipo shaka yo yote;maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo ,na kupeperushwa huku na huku.  
Mungu aliyeziumba mbingu na nchi na akujibu sawasawa na vilevile alivyoachilia ndani ya yesu sawasawa na ukarimu wake wote na iwe kwako sawasawa na isaya 11:2 katika jina la yesu upokee unayohitaji
“Isaya11:2 naroho wa bwana atakaa juu yake ,roho ya hekima na ufahamu ,roho ya shauri na uweza ,roho ya maarifa na kumcha bwana”
v  ROHO WA KWELI
“Yohana 14:17 ndiye Roho wa kweli ambae ulimwengu hauwezi kumpokea  kwa kuwa haumwoni wala haumtambui maana anakaa kwenu naye atakuwa ndani yenu”
v  ROHO MTAKATIFU KAMA MSAIDIZI KUTOKA MBINGUNI
Yohana 14:26 “lakini huyo msaidizi,huyo Roho Mtakatifu ambaye baba atampeleka kwa jina langu atawafundisha na kuwakumbusha yote niliyowaambia”.
Mungu alipochukua mwili  tukamwelewa zaidi yesu kristo alisema mimi na baba tu umoja (yohana 1:1)inaeleza yesu alikuwepo tangu mwanzo na katika yeye  vitu vyote viliumbwa  na 1wakoritho 1:17yesu ni mojawapo ya nafsi ya mungu
Bwana yesu aliwaeleza wanafunzi wake habari ya uttendaji wa RohoMtakatifu kwamba ameeandaa habari zijazo  ameeandaa na atatuletea habari kutoka kwa mungu na atamtukuza Bwana  Yesu kwa sababu ni umoja na pamoja wanatenda kazi kwa umoja.
 Pia Roho Mtakatifu atashuhudia kwa habari ya dhambi haki na hukumu .kwa habari ya dhambi ni kwa sababu ya kutomwamini yesu kristo kama mwana wa mungu aichukuae dhambi ya ulimwengu kwa ajili ya ukombozi wa watu wote.kwa habari ya haki kwa sababu yesu amepaa mbinguni na  kwa habari ya hukumu kwa sababu mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.
Matendo ya mitume 1:8 bwana yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa “mtapokea nguvu akiisha kuwajilia Roho Mtakatifu nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika yerusalemu na katika uyahudi wote na samaria na hata mwisho wan chi”  
Tangu siku za yohana ufalme wa Mungu unatekwa na wenye nguvu tena nguvu za rohoni (nguvu za ROHO mtakatifu) unapomwamini Yesu Roho Mtakatifu 

  • RAFIKI MUNGU NI PENDO ANAKUPENDA SANA TUBU DHAMBI ZAKO ZOTE YEYE NI MWAMINIFU ATAKUSAMEHE INAWEZEKANA UNATAMANI KUPATA KIPAWA HIKI CHA ROHO MTAKATIFU LEO NI SIKU YAKO NA NI KUSUDI LA MUNGU WEWE UPOKEE UZIMA TENA UDUMUO MILELE
  • WAWAWEZA KUFUATISHA MANENO HAYA YAFUATAYO KWA KUTAMKA AMBAYO NI MAOMBI KWA AJILI YA TOBA NA UZIMA WA MILELE

 MAOMBI YA REHEMA NA TOBA
SEMA ;
BWANA YESU MIMI NI MWENYE DHAMBI NAKUJA LEO MBELE ZAKO WEWE MUNGU WANGU NATUBU DHAMBI ZANGU LEO, NILIZOFANYA KWA KUWAZA KUTENDA  KWA KUKUSUDIA NA KUTOKUKUSUDIA NINAOMBA UNISAMEHE NA UNISAFISHE ROHO YANGU,NAFSI YANGU NA MWILI WANGU KWA DAMU YAKO 
FUTA JINA LANGU KWENYE KITABU CHA HUKUMU NA ANDIKA JINA LANGU KWENYE KITABU CHA UZIMA,TANGU SIKU YA LEO NIONGOZE TAWALA MOYO WANGU ,UFAHAMU WANGU NA KILA NIKIFANYACHO NIONGOZE KATIKA UPYA WA MAISHA  KWA ROHO WAKO MTAKATIFU .TANGU LEO MIMI NI MTOTO WA MUNGU NILIYEZALIWA KATIKA MUNGU KWA UWEZO WA ROHO MTAKATIFU TANGU LEO NIMEOKOKA 

  • YAWEZEKANA MAHALI ULIPO UNATESWA NA NGUVU ZA GIZA ,MAGONJWA ,UTASA,NDOTO MBAYA ,HUZUNI NA UCHUNGU MOYONI,MOYO UNAUMA AU UNA UVIMBE TUMBONI MWAKO,HAUFANIKIWI ,WATOTO WAKO WAMEKUWA MWIBA KWAKO,NDOA YAKO IMEKUWA MWIBA KWAKO,UNATESWA NA NGUVU ZA KICHAWI AU MAJINI NA MAPEPO,UNATESWA NA MIZIMU,UNA UKIMWI ,HUONI SIKU ZAKO(WANAWAKE)UNAUMWA MADAKTARI HAWAONI UGONJWA NDANI YAKO, LEO NI SIKU YAKO YA KUPOKEA MUUJIZA  WAKO 
  • WAWEZA KUFUATISHA KWA SAUTI NDOGO HUKU IMANI YAKO UKIELEKEZA KWA MUNGU JEHOVA MPONYAJI YEYE NI BABA TENA NI MUNGU WA WOTE WALIO NA MWILI WEKA MKONO WAKO WA KULIA KIFUANI MWAKO KISHA OMBA MAOMBI HAYO HAPO CHINI NA MUNGU WANGU ATAACHILIA UZIMA NDANI YAKO LEO.
  • MAOMBI YA UPONYAJI
  • BWANAYESU NINAKUTUKUZA NA KUKU TUKUZA WEWE NI MPONYAJI TENA NI MUNGU MWENYE NGUVU BABA KATIKA JINA LA YESU NINAOMBA UNIPONYE...........(TAJA UNACHOUMWA)
  • .NINAKATAA LEOMATESO YA MAJINI,UCHAWI,MAPEPO NA KILA AINA YA MATESO NINAKUAMURU SHETANI ACHILIA NYOTA YANGU,ACHILIA UCHUMI WANGU ACHILIA AFYA YANGU ACHILIA ACHILIA NDOA YANGU ACHILIA MAISHA YANGU,TOWEKA KWA JINA LA YESU  UTASA MAGONJWA NA LAANA KATIKA MAISHA YANGU 
  • NATUMIA MOTO WA ROHO MTAKATIFU KUTEKETEZA KILA AINA YA NGUVU ZA GIZA ZILIZOJIPANGA KUNIVAMIA KATIKA JINA LA YESU
  •  KATIKA JINA LIPITALO MAJINA YOTE KWA JINA LA YESU NATANGAZA UZIMA NDANI YANGU MIMI NIPOHURU KWA JINA LA YESU,MIMI NI MZIMA NAKUTUKUZA BWANA YESU KWA KUNIPONYA KATIKA JINA LA YESU
  •  UMESAMEHEWA NDUGU YANGU TANGU LEO WEWE NI MWANA WA MUNGU WAWEZA TAFUTA KANISA LILILO KARIBU NA MAZINGIRA YAKO NENDA KAWAELEZE KUWA UMEOKOKA KUPITIA BLOG HII MUNGU WANGU NA AKUBARIKI 
  • JE KUNA KITU MUNGU AMEFANYA KWAKO KUPITIA SOMO HILI USIACHE  KUSHUHUDIA KATIKA SANDUKUHILO HAPO CHINI WEKA KOMENT YAKO PIA WATUMIE RAFIKI ZAKO UWAPENDAO MAANA HIZI NYAKATI ZA WOKOVU KWA WOTE
  •  KUNIANDIKIA KATIKA EMAIL HII


0 comments: